Kabla ya kuanza ujenzi wa viwanja vya michezo na maeneo rasmi ya mazoezi, Mgombea Urais wa CCM Zanzibar mwaka 2020, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alikutana na wanamichezo katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba kwa lengo la kusikiliza changamoto sugu walizokuwa wakikabiliana nazo na kufahamu mazingira halisi ya michezo Zanzibar.
Kipindi cha kampeni za Urais za mwaka 2020, Dkt. Hussein Ali Mwinyi hakutilia mkazo hotuba ndefu majukwaani, bali aliamua kushuka mitaani, kukutana na wanamichezo, makocha na mashabiki. Aliahidi si tu kuboresha mazingira ya michezo, bali pia kuwezesha ndoto za wanamichezo wa Zanzibar kutimia.
Picha hii ni ushahidi wa Uongozi Unaoacha Alama. Kwa bashasha na ukaribu, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alikutana na wadau mbalimbali wa michezo, akashiriki nao mchezo wa mpira wa mikono, na hatimaye kuwaahidi kuwa siku za matumaini kwa maendeleo ya sekta ya michezo Zanzibar zinakuja.