LONDON: MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta amesema mabeki wake walikuwa hawana akili ya kiulinzi baada ya kikosi chake kupoteza mchezo mwingine wa kirafiki kwa mabao 3-2 dhidi ya Villarreal katika dimba lao la nyumbani la Emirates.
Arsenal, ambao walianza maandalizi yao kwa msimu mpya kwa ushindi dhidi ya AC Milan na Newcastle United kabla ya kupoteza kwa mahasimu wao wa London Tottenham Hotspur walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 ndani ya dakika 33 dhidi ya moja ya klabu katili za hispania Villarreal usiku wa Jumatano.
“Nadhani matokeo ya leo ni machungu kwa kila mtu. Nadhani (Villareal) walikuwa na ufanisi mkubwa lakini sisi tumekuwa kama hatuna akili haswa kwa jinsi ambavyo tumejilinda katika nafasi za wazi na hilo ni jambo ambalo ni lazima tulishughulikie haraka sana. Leo hatujawa wazuri kabisa katika idara hiyo (Idara ya ulinzi) na ni wazi hilo limetugharimu mchezo” Arteta aliwaambia waandishi wa habari.
Arteta, hata hivyo, alifurahishwa na kile alichokiona kutoka kwa mshambuliaji wake mpya Viktor Gyokeres ambaye alikamilisha usajili wake kutoka Sporting mwezi uliopita baada ya kumpa msweeden huyo mwenye umri wa miaka 27 nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye cha Arsenal.
“Nadhani ilikuwa muhimu sana kwake kuanza katika mechi hii na kuanza kuwa na hisia na uhusiano na timu,” Arteta alisema.
The post “Mabeki wangu hawana akili” – Arteta first appeared on SpotiLEO.