DAR ES SALAAM: MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mudathir Yahya amesema kuwa pamoja na changamoto zinazowakumba uwanjani, bado wanaendelea kupambana kwa hali na mali ili kuipa heshima nchi.
Akizungumza baada ya mechi ngumu dhidi ya Mauritania kwenye mashindano ya kimataifa, Mudathir alikiri kuwa bado hawajafikia matarajio ya Watanzania, lakini alisisitiza kuwa kikosi hicho hakijakata tamaa.
“Michezo ni migumu, lakini tutaendelea kupambana hatua kwa hatua. Bado tuna deni Stars kwa Watanzania,” alisema kiungo huyo mahiri aliyeibuka mchezaji bora katika mchezo dhidi ya Madagascar.
Katika mchezo huo wa Jana michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na hivyo imebakiza michezo miwili dhidi ya Madagascar na Central Afrika kuhitimisha hatua ya makundi.
Inahitaji sare zote au ushindi wa mchezo mmoja kupenya hatua ya robo fainali.
Mudathir ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha sasa cha Taifa Stars kinachotarajiwa kufanya vizuri kwenye michezo ya kufuzu AFCON na Kombe la Dunia, huku mashabiki wakitarajia kuona kiwango cha juu kutoka kwa nyota hao.
Kauli hiyo inakuja wakati Taifa Stars ikikabiliwa na presha ya kufanya vizuri ili kurejesha imani ya mashabiki, hasa baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya awali.
The post Mudathir: Bado Tuna Deni kwa Watanzania first appeared on SpotiLEO.