Dakika 180 za kiwango bora mbele ya kioo akitazamwa na familia , wana na wapenda mpira Afrika na Duniani kote . Alicheza kwa kiwango cha juu dhidi ya Burkina Faso na leo amecheza maradufu zaidi dhidi ya Mauritania
Zanzibar Greatest ametunukiwa kuwa MAN OF THE MATCH na kila aliyetazama mchezo ameridhika amefanya mizunguko mingi yenye tija akiunganisha eneo la ushambuliaji na eneo la kujilinda
Ameshambulia ilipohitajika , amepika ilivyobidi kufanya hivyo na alishuka kuzuia kulinda usalama wa Taifa