LOS ANGELES: RAIS wa Marekani Donald Trump ameunda kikosi kazi ambacho atakiongoza kwenye Michezo ya Olimpiki ya 2028 Los Angeles, jiji linaloongozwa na chama cha Democrat ambao ni wapinzani kwa chama cha Republican.
Kundi hilo litashirikisha serikali ya shirikisho ili kuhakikisha Michezo ni salama na ina mafanikio ya kihistoria, ambayo inaweza kumpa rais Trump na washirika wake ushawishi mkubwa katika michezo.
Trump atahudumu kama mwenyekiti na Makamu wa Rais JD Vance atakuwa makamu mwenyekiti wa kikosi kazi hicho, ambacho kitajumuisha viongozi wengine kadhaa katika utawala wake.
Akitia saini agizo la kuanzisha kikosi hicho, Trump amesema: “Tutafanya chochote kinachohitajika kuweka michezo ya Olimpiki salama, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kupeleka walinzi wetu wa kitaifa au jeshi.”
Trump alidai kutumwa huko ni muhimu ili kuzima maandamano ambayo yalikuwa yamepamba moto dhidi ya uvamizi wa wahamiaji wa shirikisho huko Los Angeles, ambayo ina idadi kubwa ya wahamiaji.
The post Trump ‘miguu miwili’ Olimpiki ya Los Angeles first appeared on SpotiLEO.