LONDON: Klabu ya West Ham inayoshiriki ligi kuu ya Egland imetangaza kuachana na Mshambuliaji wake raia wa Jamaica Michail Antonio baada ya mkataba wake kutoongezwa kufustis kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alihusika katika ajali mbaya ya barabarani mwezi Desemba mwaka jana wakati gari lake lilipogonga mti alipokuwa akirejea nyumbani kutoka mazoezini na kuvunjika mfupa wa paja mara nne na hakuichezea West Ham tena.
“Michail siku zote atakuwa mwanafamilia anayependwa na kuheshimika sana na familia ya West Ham United. Kama ilivyokuwa tangu Desemba, Klabu itaendelea kumuunga mkono na kumsaidia katika kila hatua ya kupona kwake kwa kumpa fursa ya kufanya mazoezi, vifaa na matibabu ikiwa itahitajika,” West Ham imesema katika taarifa yake.
“Mazungumzo yanaendelea kuhusu uhusika wake klabuni hapa kwa siku za usoni ikiwa ni pamoja na hatua ambayo itawawezesha wengine kufaidika na uzoefu wake na sifa zake za uongozi na siku zote atakuwa na nafasi maalum katika historia yetu ya miaka 130.” – imeendelea taarifa hiyo.
Antonio aliisaidia West Ham kushinda Ligi Conference mwaka 2023, na kumaliza ukame wao wa miaka 43 bila taji. Antonio alirejea mwezi Juni kama mmchezaji wa akiba wa Jamaica katika mchezo wa Kombe la CONCACAF dhidi ya Guatemala.
Antonio alijiunga na klabu hiyo ya London kutoka Nottingham Forest mwaka 2015 na kucheza mechi 323, akifunga mabao 83 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa West Ham kwenye Premier League.
The post West Ham watemana na Antonio first appeared on SpotiLEO.