DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga ya Tanzania imeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya vifaa vya kieletroniki vya majumbani kutoka China, HAIER wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.3.
Udhamini huo utawezesha logo ya Kampuni hiyo kukaa kwenye bega la kushoto la jezi za Yanga kwa miaka mitatu.
Akitangaza kuendeleza mahusiano na Kampuni hiyo leo Agosti 7, 2025 Dar Es Salaam, Rais wa klabu hiyo Hersi Said amesema Mkataba wa awali na Haier ulikuwa mzuri sana na ulikuwa na baraka kubwa iliyopelekea kufanya vizuri kwenye mashindano ya shirikisho ambapo klabu hiyo ilifika fainali.
“Ni matumaini yetu kuwa mkataba huu mpya utakuja na mafanikio zaidi. Msimu wa kwanza na Haier tulifika fainali ya Shirikisho Afrika. Mkataba huu utakuwa wa miaka mitatu mpaka mwaka 2028,”amesema.
Leon Chi, Mkurugenzi wa Kanda wa kampuni hiyo amesema: “nimejivunia kuwa sehemu ya watu ambao wamewezesha mahusiano baina ya Haier, GSM na Yanga.
” Nawashukuru sana kwa mchango wao mkubwa kwenye kutangaza bidhaa za Haier na nembo yetu kiujumla. Ni matarajio yetu mahusiano haya yatadumu na kuwa na tija kwa siku zijazo,” amesema.
Meneja wa kampuni hiyo Ibrahim Kiongozi amesema mahusiano ya Haier, Yanga na umeleta mapinduzi makubwa.
” Leo tumekuja kutangaza kuwa tunaendelea na mahusiano ambayo yamekuwa na manufaa kwa pande zote tatu,” amesema.
The post Yanga yaongezewa donge nono first appeared on SpotiLEO.