DAR ES SALAAM, Matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam FC wamepangwa kupepetana na timu ya El Merreikh Bentiu ya Sudan katika hatua ya kwanza ya raundi ya awali ya kombe la Shirikisho barani Afrika katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wakati Azam FC wakivaana na wababe hao kutoka Sudan wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano hiyo Singida Black Stars watasafiri hadi jijini Kigali kuvaana na mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Rwanda Rayon sports katika hatua kama hiyo.
Wawakilishi wa Zanzibar katika michuano hiyo KMKM wao watajitetea mbele ya AS Sport kutoka nchini Djibouti.
Mshindi kati ya Azam FC na atavana na mshindi kati ya KMKM na AS Sport Huku mshindi kati ya Singida Black Stars na Rayon Sports akivaana na Mshindi kati ya Flambeau Du Centre ya Burundi na timu moja kutoka Libya itakayofahamika baadaye.
Michezo ya raundi ya kwanza ya hatua ya awali inatarajiwa kupigwa kati ya Septemba 19-21 na marudiano kati ya tarehe 26-28 na michezo ya raundi ya pili ya hatua hiyo itapigwa kati ya Oktoba 17-19 na marudiano wiki moja baadaye
Michuano ya msimu huu imekuja na sura mpya baada ya kuhusisha takribani klabu za mpira wa miguu 120 kutoka kote barani Afrika.
The post Azam, Singida kuanzia ugenini CAFCC first appeared on SpotiLEO.