DAR ES SALAAM, WANA FAINALI wa kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita wekundu wa Msimbazi Simba Sports club watavaana na Gaborone United ya Botswana katika hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baadaye mwezi Septemba
Simba klabu namba 5 kwa ubora katika orodha ya CAF wanaingia katika michuano hiyo kuthibitisha ubora huo na kushikilia kiwango chake na kuthibitisha ubora wake katika soka la Klabu barani Afrika
Ikiwa wekundu wa Msimbazi wataibuka washindi katika mechi hiyo itavaana na mshindi kati ya Simba Bhora ya Mozambique na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini
Michezo ya raundi ya kwanza ya hatua ya awali inatarajiwa kupigwa kati ya Septemba 19-21 na marudiano kati ya tarehe 26-28 na michezo ya raundi ya pili ya hatua hiyo itapigwa kati ya Oktoba 17-19 na marudiano wiki moja baadaye
The post ‘Mai’ wa Simba CAFCL huyu hapa first appeared on SpotiLEO.