
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Habib Kyombo, amejiunga rasmi na Mbeya City kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars.
Kyombo, mwenye umri wa miaka 24, raia wa Tanzania, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka katika kikosi hicho cha Ligi Kuu Bara hadi Juni 2027.
Usajili wa Kyombo unatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Mbeya City kuelekea msimu mpya wa 2025/26.