Mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge, Hayati Job Yustino Ndugai, umefikishwa nyumbani kwake Njedengwa Jijini Dodoma kwa ajili ya taratibu za kifamilia jioni leo tarehe 09 Agosti, 2025.
Shughuli ya kumuaga Hayati Ndugai itafanyika kitaifa kesho tarehe 10 Agosti, 2025 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na baadaye kupelekwa Wilayani Kongwa kwa ajili ya taratibu za mazishi.