Mshambuliaji wa Yanga SC Clement Mzize bado anaendelea kuzigonganisha Klabu kubwa Barani Afrika juu ya kuhitaji Huduma yake.
Hadi sasa Yanga Tayari ina makubaliano na Klabu ya Al-Sadd SC ya Qatari lakini Klabu hiyo bado haijafikia makubaliano na menejimenti ya Mchezaji hasa juu ya Mshahara wa Mchezaji huyo.
Timu za Al Masry, Zamalek na Al Ittihad ya Libya nazo zilituma Ofa ambazo hata hivyo hazikumshawishi Mchezaji huyo upande wa Maslahi.
Vigogo wa Tunisia Esperance De Tunis inatarajiwa kutuma Ofa Rasmi Ndani ya Siku chache zijazo kujaribu Kumshawishi Mzize kuelekea Nchini Tunisia.
Uongozi wa Young Africans Tayari Umefungua milango kwa Mzize Kwenda Kutafuta Changamoto nje ya mipaka ya Tanzania , lakini Taarifa za uhakika zinasema Kinachokwamisha Hadi sasa ni Upande wa Wasimamizi wake.