
Bwanashamba elekezi kutoka kampuni ya ZAMSEED, Emmanuel Buseluka akielezea namna mbegu hiyo ya mahindi inavyoleta tija kwa wakulima
Na Hellen Mtereko,Mwanza
WAKULIMA nchini wametakiwa kuachana na dhana ya kulima kimazoea pamoja na matumizi ya mbegu zisizo na ubora, na badala yake wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu za kilimo bora ili kufanikisha uzalishaji wenye tija.
Hayo yamebainishwa na Bwana Emmanuel Buseluka, Bwana Shamba Elekezi kutoka Kampuni ya ZAMSEED, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nyamhongolo, Jijini Mwanza.
Amesema ili mkulima aweze kulima kilimo chenye tija inatakiwa azingatie vitu vitatu ambavyo ni mbegu bora,lishe linganifu kwenye mmea ikiwemo mbolea ya kupandia,kukuzia na kuzalishia pamoja na udhibiti wa wadudu waharibifu.
“Tunambegu tano hapa Tanzania ambazo ni ZAMSEED 405,520,606,638 na 721 na zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni mbegu za muda mrefu,wakati na wachini”, Amesema
Alieleza kuwa Mbegu ya ZAMSEED 405 ni mbegu ya miezi miwili hadi miwili na nusu na inauwezo wakutoa gunia 20 hadi 25, 520 ni mbegu ya miezi miwili na nusu hadi mitatu inatoa gunia 30 hadi 35 kwa hekari,606 ni ya miezi mitatu hadi mitatu na nusu na inatoa gunia 30 hadi 35,638 mbegu ya kati kuelekea muda mrefu inakomaa kwa miezi mitatu na nusu hadi minne na inauwezo wakutoa gunia 35 hadi 40 na ZAMSEED 721 ni mbegu ya muda mrefu na inawafaa watu wa nyanda za juu kusini na inauwezo wa kutoa gunia 40 hadi 45.
“Mkulima akifuta taratibu zote za kilimo na akatumia mbegu za ZAMSEED atakuwa amelima kilimo chenye tija ambacho kitamuinua kiuchumi”, Amesema Buseluka