KAMA unadhani Yanga SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamemaliza usajili, bado kazi haijaisha kwa kuwa kuna wachezaji wengine wapya bado hawajatambulisha.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa mara 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hii ni ligi namba nne kwa ubora Afrika.Ni pointi 82 Yanga SC ilikusanya baada ya mechi 30 mafasi ya pili ipo mikononi mwa Simba SC yenye pointi 78 kibindoni.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa bado hawajamaliza usajili kwa msimu wa 2025/26. Tayari Yanga SC imetambulisha wachezaji 9 wapya akiwemo beki wa kushoto Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Offen Chikola.
Zimbwe Jr alikuwa nahodha wa Simba SC msimu wa 2024/25. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye changamoto mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kimeweka kambi Dar na kinatarajiwa kuelekea Rwanda kati ya Agosti 13 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayor Sportt.
Kamwe amesema: “Bado hatujamaliza usajili na kuna wachezaji kama watatu hivi tutamalizana nao na kuwatambulisha. Tunahitaji kuwa na kikosi imara chenye ushindani mkubwa hilo lipo wazi.”