Kiungo mpya wa Simba SC Mohamed Bajaber kwenye mahojiano na Idara ya Habari Simba akielezea hali yake baada ya kupata ofa ya Simba SC
“Nilikuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa nikiwa na majeraha nikawa napima kama naweza kucheza CHAN au niende Simba , kwa sababu ofa ya Simba ni fursa kubwa nikaona acha niache CHAN nije Simba , hiyo siku sikulala kabisa , nilikuwa nafikiria usiku kucha niko peke yangu chumbani”
“Sikulala kwa sababu Simba ni timu kubwa na ni fursa kubwa kwangu , mimi sijawahi kabisa kucheza mbele ya mashabiki wengi ukiacha mechi moja ya timu ya Taifa dhidi ya Gambia so nikawa nafuraha sana kwa sababu nataka kucheza timu yenye mashabiki wengi na ni kitu poa kuwafurahisha mashabiki wengi”