Rotary Club Oysterbay Dar es salaam ikishirikiana na wadau mbalimbali wa afya na wafadhili, wanatoa huduma ya Matibabu bure ikiwemo upimaji,Saratani ya uzazi ,tezi dume, macho,Malaria,masikio, VVU na ushauri nasaha katika Shule ya Msingi Mzambarauni iliyoko Ukonga Jijini Dar es salaam .
Akizungumza na Waandishi Agosti 9,2025 Jijini Dar es salaam Muandaji wa Kambi ya Matibabu Ukonga Hilu Bura amesema zoezi hilo limepokelewa vizuri kwani walijiwekea lengo la kuhudumia watu Elfu tatu miatano lakini mpaka sasa wanakaribia na kufika lengo hadi kuzidi
” Tumekuja na Madaktari bungwa wanawake na wanaume wanatoa Matibabu ya meno ,ngoz,i masikio,macho hivyo tumechagua kusaidia Jamii kwa upande wa Afya kwa kuwa tunatambua siyo wote wanaoweza kumudu gaharama za Matibabu”amesema Hilu
Kwa Upande wake Makamu wa rais wa Rotary Club Tanzania Paul Muhato amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa huduma huo ni Mwaka nane kuisaidia jamii kwa kushirikiana na Wadhamini mbalimbali ikiwemo Pepsi ,CCBRT,SGA
“Tumefanya hii huduma tangu 2018 masala ya Afya NI moja ya kipaumbele chetu ila pia tunasaidia masuala ya Elimu na tunatoa huduma hii mara mbili kwa Mwaka tuna watu Zaidi ya Milioni tatu ambao wamekuwa wakijitole kuisaidia jamii’ Amesema Muhato
Naye Mwananchi aliyepata Matibabu Oska Khamisi ameishukuru Rotary kwa huduma ya Afya wanayoitoa bure kwani kuna Wananchi wengi hawana utaratibu kwenda Hospitali mpaka wazidiwe kutokana na kukosa fedha hivyo anaomba isiwe Leo tu iwe endelevu