Washindi wa pili wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita Simba SC wamepangwa kucheza dhidi ya timu ya Gaborone United Botswana.
Simba SC wamepangwa kuanzia ugenini kwa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na hiyo inakuwa mara ya pili kwa miaka ya hivi karibuni Simba SC kupangiwa na timu za nchini humo.
Mara ya mwisho Simba SC ilipangwa na timu ya Jwaneng Galaxy na iliondolewa mashindanoni kwa faida ya mabao ya ugenini.