Mshambuliaji na nyota wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amemrushia maua yake mchezaji mpya wa Arsenal, Viktor Gyokeres akimuita mwanasoka ‘Special’.
Gyokeres alihamia Arsenal akitokea Sporting ambapo alifunga mabao 97 katika mechi zaidi ya 100 alizocheza na klabu hiyo kwenye mashindano yote.
Hata hivyo, Ronaldo, ambaye pia alianza soka lake la kulipwa katika klabu ya Sporting, alisisitiza kwamba klabu yake ya zamani itabakia klabu bora yenye ushindani licha ya Gyokeres kuondoka.
“Siku zote huwa naitakia mema Sporting na wanaweza kuwa mabingwa tena,” Ronaldo alinukuliwa na Metro UK akisema.
“Viktor alikuwa mchezaji wa kipekee, lakini Sporting italazimika kuzoea.” alimalizia Ronaldo.