Kuna namna wachezaji wa kigeni wenye ubora wanavyozidi kuja kwenye ligi yetu na ubora wa wachezaji wazawa unaongezeka! Inawezekana ile hoja ya kuruhusu wachezaji wachache wa kigeni ili wachezaji wa ndani wapate nafasi zaidi kwenye klabu kubwa (Simba/Yanga) haikua na mashiko
Wapo wazawa waliojipambanua kwenye klabu hizohizo kubwa wakapata namba na mwisho wa siku wanaonyesha ubora mkubwa sana kwenye timu yetu ya taifa.
Kwa tathmini fupi Mtizame Mudathir, Ibra Bacca kisha mtizame shomari na Zimbwe Jr ambae kawakimbiza ma-pro kibao kwenye namba yake….mtizame Feisal ambae alikua anapata nafasi mbele ya Azziz Ki pale Yanga….uwezo unajieleza
Kuna namna klabu ya Azam ambayo inalisha soka la Tanzania kwa asilimia kubwa ya wachezaji kutoka kwenye mifumo yake ya soka la vijana imeleta wachezaji muhimu kama Sopu na mpishi wa mabao Nado!
Huenda kufanya vizuri kimataifa kwa klabu zetu imekua chachu ya kuwa na ligi bora? Na pia wachezaji wetu wa ndani kuimarika kwa kiasi kikubwa?
Majibu yatasalia kwenye hatua tutakayofika kwenye michuano hii ya CHAN. Ila mpaka kufikia sasa naona hata benchi la ufundi lipo na wazawa kwa 90%.