
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDA’s na LGA’s), ametangaza nafasi 199 za ajira mpya na kuwataka Watanzania wenye sifa na uwezo kuwasilisha maombi yao.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, nafasi hizo zimetolewa kwa ajili ya kada mbalimbali na zitajazwa kulingana na mahitaji ya taasisi husika. Maelezo ya kina kuhusu masharti, sifa, na jinsi ya kuomba yameelezwa katika tangazo rasmi lililotolewa na Sekretarieti ya Ajira.
Waombaji wote wanashauriwa kuzingatia maelekezo ya tangazo na kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa ajira wa Serikali ndani ya muda uliopangwa.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 22 Agosti, 2025
BONYEZA HAPA >>> TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MDAs NA LGAs