SIMBA SC bado ipo sokoni kusaka wachezaji wapya kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kikosi cha Simba SC kwa sasa kipo Misri kwa maandalizi ya msimu mpya ambapo inaelezwa kuwa huenda Joshua Mutale akaachwa kuelekea msimu mpya kupisha nafasi ya mchezaji mpya.
Mbali na Mutale, Leonel Ateba naye yupo kwenye hesabu za kuachwa na Simba SC kutokana na mwendo wake kutokuwa imara kwa msimu uliopita.
Eneo ambalo Simba SC kwa sasa inafanyia kazi ni beki wa kushoto mgeni atakayeongeza nguvu eneo hilo ambalo Mohamed Hussen Zimbwe Jr ameondoka.
Zimbwe Jr yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC akiibukia huko baada ya mkataba wake na Simba SC kuisha hivyo kaibuka hapo akiwa ni mchezaji huru.