Timu ya Taifa ya Afrika Kusini imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN2024 baada ya kuilaza Guinea 2-1 katika dimba la Mandela, Kampala Uganda.
Afrika Kusini imefikisha pointi nne baada ya mechi mbili huku ikikwea mpaka nafasi ya pili nyuma ya Algeria wenye pointi nne pia. Uganda The Cranes wapo nafasi ya tatu alama tatu baada ya mechi mbili huku Guinea wakiwa nafasi ya nne alama tatu baada ya mechi tatu wakati Niger ikiburuza mkia bila alama yoyote.
FT: South Africa 🇿🇦 2-1 🇬🇳 Guinea
⚽ 10’ Maema
⚽ 54’ Kutumela
⚽ 37’ Camara