NAIROBI: UUZAJI wa tikiti za baadhi ya mechi za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) jijini Nairobi umesitishwa baada ya matukio ya fujo kutokea baada ya ushindi wa Kenya dhidi ya Morocco siku ya Jumapili.
Kutokana na hilo mashabiki 27,000 pekee ndiyo wataruhusiwa kuhudhuria mechi za Kenya katika Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi (MISC) chenye uwezo wa kuchukua watu 48,000 (MISC) Kasarani, jijini Nairobi wakati wa michuano inayoendelea ya Mataifa ya Afrika 2024.
Harambee Stars ilishinda bao 1-0 kwenye uwanja uliojaa wa Kasarani, lakini matokeo yalitawaliwa na fujo ndani na nje ya uwanja kabla na wakati wa mechi hiyo.
Ukiukaji huo wa usalama ni pamoja na lango lililovunjwa, mashabiki kuingia bila kulipia, msongamano zaidi ya uwezo wa watu 48,063 na uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vyombo vya habari.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia uwanjani kutoka lango la chini wameshutumu polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mookh Africa, mtoa huduma wa tikiti wa CHAN nchini Kenya, aliithibitishia kwamba mauzo ya mechi zijazo katika uwanja huo, unaojulikana rasmi kama Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi, yamesitishwa hadi waandaaji watoe maagizo zaidi.
Kamati za nidhamu na usalama za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) zimeanzisha uchunguzi lakini msemaji wa shirikisho la mchezo huo wa bara alikanusha kuwa limechukua uamuzi wa kusimamisha mauzo.
“Caf ina wasiwasi kuhusu hali ya usalama inayoshuhudiwa katika michezo ya Kenya,” msemaji huyo alisema.
“Caf inashirikiana na kamati andalizi ya eneo hilo na serikali (ya Kenya) kushughulikia masuala ya usalama.”
Tukio hilo lilikuja siku chache baada ya FKF kupigwa faini ya dola 20,000 na Caf, nje na dola 2,500 ya kiasi hicho kusimamishwa, kwa udhibiti wa umati wa watu mapema na kushindwa kwa usalama katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yanafanyika kwa ushirikiano wan chi tatu Tanzania, Kenya na Uganda.
The post CAF yapunguza idadi ya mashabiki wa Kenya uwanja wa Kasarani first appeared on SpotiLEO.