Baada ya miaka 9 ya kuwa kwenye mahusiano, nguli wa soka Cristiano Ronaldo amemvalisha rasmi pete ya uchumba mpenzi wake Georgina Rodriguez, hii ikimaanisha kuwa ndoa ya wawii hao inanukia.
Ronaldo na Rodriguez wana watoto wanne pamoja mapacha Eva Maria na Mateo (aliyezaliwa 2017), Alana (aliyezaliwa 2017) na Bella (aliyezaliwa 2022). Kwa bahati mbaya, pacha wa Bella alikufa mwaka 2022.
Wanandoa hao pia wanaishi na mtoto mkubwa wa Ronaldo, Cristiano Ronaldo Jr. (aliyezaliwa mwaka 2010).