
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo, amesema ana matumaini kuwa jina lake litateuliwa kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akizungumza na wanahabari wakati wa maziko ya Hayati Job Ndugai wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, Shigongo amesema anaamini matokeo ya ushindi wake kwenye kura za maoni na uhitaji mkubwa wa wananchi dhidi yake vitamwezesha kuaminiwa tena kupeperusha bendera ya chama hicho.
Aidha, Shigongo amesema kifo cha Ndugai, Taifa limepoteza mtu muhimu ambaye anapaswa kukumbukwa kwa mema mengi aliyoyafanya kuliko madhaifu.