Kampuni ya michezo ya kubashiri, SportPesa, imeingia mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Yanga wenye thamani ya Shilingi Bilioni 21.7.
Kwa mujibu wa mkataba huo, Yanga itavuna Shilingi Bilioni 7.2 kila mwaka, ndani ya kipindi cha miaka hiyo mitatu.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa SportPesa, Abass Tarimba, alisema kuwa mbali na fedha hizo za udhamini, wameandaa zawadi ya kipekee endapo Yanga itatwaa Ubingwa wa Afrika.
“Tumepanga donge nono ambalo hakuna klabu iliyowahi kupata endapo Yanga watabeba Ubingwa wa Afrika,” alisema Tarimba.
Mkataba huu unaimarisha uhusiano kati ya SportPesa na Yanga, ambao tayari umekuwa sehemu ya historia ya mafanikio ya klabu hiyo katika soka la Tanzania na Afrika.