Mwenge wa Uhuru unatarajia kuanza mbio zake Mkoani Mara August 15 mwaka huu, ukitokea Mkoani simiyu ambapo utatembelea na kukagua,kuweka mawe ya Msingi,kufungua na kuzindua Miradi 68 ya Maendeleo ya wananchi katika Halmashauri Tisa za Mkoa huo yenye thaman ya shilingi Bilioni 26.54.
Mkuu wa Mkoa wa mara Kanali Evans Mtambi akizungumza na wandishi wa habari alisema Mwenge huo wa Uhuru urawasili Mkoani Mara ukitokea Mkoani simiyu na utakimbizwa kwa Takribani km 1123 katika Mkoa wa Mara ambapo utatembelea na kukagua ,kuweka mawe ya msingi,kufungua na kuzindua Miradi 68 ya Maendeleo ya wananchi katika Halmashauri zote tisa za Mkoa huo wa mara Miradi ikiwa na thaman ya shilingi Bilioni 26,547,598,285.42.
Amesema Mwenge wa Uhuru utakapokuwa Mkoani mara nisharti uzuru nyumbani kwa Baba wa Taifa na kuwasha Mwenge wa Mwitongo ambapo tukio hilo la kuwasha Mwenge wa Mwitongo kitakuwa Aug 18 ,2025.
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitahitimishwa Mkoani mara Aug 23 na kisha Aug 24 Mwenge wa Uhuru unakabidhiwa Mkoani Mwanza