Timu ya Azam fc muda wowote itatoa tamko rasmi la kuvunja mkataba na kipa wao raia wa Sudan Mohamed Mustafa.
Tayari maamuzi ndani ya klabu yamesha fanyika na mchakato wa kutafuta kipa mwengine umeanza mara moja. Sababu za Azam kuvunja mkataba na Mustafa ni majeraha aliyo nayo kwa sasa.
Mustafa kabla ya kupewa Mkataba alikuwa na kiwango bora sana na baada ya kupewa mkataba kiwango chake kimeshuka maradufu.
Msimu ujao Azam fc golini atakuwa nyanda Aishi Salumu Manula.