BARCELONA: MSHAMBULIAJI wa FC Barcelona Marcus Rashford amesema klabu yake ya zamani Manchester United imepoteza mwelekeo kwakuwa kuna ukosefu wa mikakati thabiti jambo linalopelekea United kuwa ‘Shamba la bibi’
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyeichezea United mara 426 baada ya kuibuliwa kutoka kwenye Akademi ya klabu hiyo awaambia wanahabari Gary Neville na Micah Richards kwenye ‘Podcast’ ya ‘The Rest is Football’ kuwa anaamini mzizi wa shida za United uko katika kutokuwa na utulivu unaosababishwa na kuteua mameneja sita tofauti tangu Alex Ferguson alipostaafu mwaka 2013.
“Tumekuwa chini mno sehemu ambayo United haistahili kuwa ukiangalia nyuma miezi sita iliopita utakubaliana na mimi unategemea nini katika hali kama hiyo”
“Wakati Liverpool wanapitia kama hii, walikuwa na (Jurgen) Klopp, walishikamana naye. Hawakuwa wakishinda mwanzoni lakini alikuwepo. Watu wanakumbuka miaka yake michache ya mwisho wakati alikuwa akishindana na Manchester City na wakati akishinda mataji makubwa kubwa”.
“Kuanza mabadiliko lazima uwe na mpango na ushikamane nao. Sio rahisi kufanya. Lakini hapa ndipo ninapozungumza juu ya kuwa na uhalisia wa hali yako. Tumekuwa na mameneja wengi tofauti wanaokuja na maoni tofauti na mikakati tofauti inayoifanya United kuwa ‘shamba la bibi’.” – amesema Rashford
United walikuwa na msimu mbovu zaidi kwa klabu hiyo tangu waliposhuka Daraja msimu wa 1973/74 wakimaliza katika nafasi ya 15 kwenye ligi wakikosa nafasi kwenye michuano ya Ulaya. Wamekuwa nje yam bio za Ubingwa tangu kuondoka kwa Ferguson zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Rashford yupo kwa mkopo Barcelona baada ya kuondoka United kwa mkopo Kwenda Aston Villa kisha kutolewa tena kwa mkopo hadi kwa mabingwa hao wa LaLiga kufuatia maelewano mabaya kati yake na meneja Ruben Amorim
The post “United imepoteza mwelekeo” – Rashford first appeared on SpotiLEO.