Pure talent kabisa huyu Denis Nkane wakati akiwa na Biashara united alikuwa hatari mno ulikuwa unaona raha kumwona kijana mdogo akicheza mpira mkubwa.
Naelewa kuhusu maslahi yake binafsi ila najaribu kuangalia project ya Yanga sc na ushindani uliopo kuanzia msimu uliopita ambao Nkane hajacheza hata mechi 10 halafu naiangalia Yanga ya msimu ujao unaona kabisa Nkane ana mazingira magumu ya kupata namba.
Ameongeza mkataba kusalia Yanga sc ila ajitathimini kama mchezaji anahitaji kucheza kwa kuonyesha kuwazidi uwezo waliopo au ana enjoy tu kukaa Yanga na baada ya msimu huu ukitamatika kama hajapata game time uwezo wake utazidi kuwa chini mno.