Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi mchezaji Naby Camara raia Guinea kuwa mchezaji wao kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Waab ya Qatar aliyojiunga nayo akitokea CS Sfaxien ya Tunisia.
Camara mwenye umri wa miaka 23 ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa kushoto na kiungo mkabaji tayari amejiunga na kambi ya Simba inayoendelea nchini Misri na alikuwepo kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Karhaba SC wikiendi iliyopita.