Klabu ya Royal Charelorioi ya nchini Ubelgiji imetuma ofa ya USD 750,000 (Tsh Bilioni 1.9) kwenda kwenye klabu ya Gor Mahia ya Kenya ili kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Kenya Austin Othiambo.
Gor Mahia bado hawaijibu ofa hiyo.Lakini kwa mujibu wa tetesi zinaeleza kuwa huenda miamba hiyo ya Kenya ikamruhusu nyota huyo kuondoka baada ya michuano ya CHAN.