Timu ya Mamelodi Sundowns imemuaga rasmi mchezaji wao, Neo Maema aliyetumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka 4.
Kwa sasa, Maema yupo kambini na timu ya taifa ya Afrika Kusini kwenye michuano ya CHAN, akisubiri mashindano hayo kumalizika ili ajiunge na kambi ya klabu yake mpya.
Duru mbalimbali za habari zimekuwa zikiripoti kiungo huyo yupo mbioni kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba, kuja kuongeza nguvu kwenye nafasi ya kiungo.