

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, anatarajiwa kuchukua fomu ya kuwania urais leo Ijumaa, Agosti 15, 2025 saa 9:30 alasiri.
Shughuli hiyo itafanyika katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo jijini Dodoma.