Manchester United wanapanga mpango wa pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Sporting na Denmark Morten Hjulmand, 26, iwapo watamkosa mchezaji wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 Carlos Baleba. (Sun)
Tottenham wana imani kwamba wameweka pamoja dili la Eberechi Eze, 27, ambalo litawaridhisha Crystal Palace , ambao wanamthamini kiungo wao wa kati wa England kwa pauni milioni 68. (Team Talk)
Fulham wanaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Denmark, Rasmus Hojlund, huku AC Milan pia wakifuatilia mpango wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)
Chelsea wanapiga hatua katika juhudi zao za kumnunua Alejandro Garnacho, 21, kutoka Manchester United na wanaamini kwamba £35m ni bei nzuri kwa winga huyo wa Argentina. (Team Talk)
Arsenal wako tayari kufikiria ofa kwa mlinzi wa kushoto wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28, huku Porto , Fenerbahce na Real Betis wakimtaka. (CaughtOffside),
Borussia Dortmund wameungana na Bayer Leverkusen kuonyesha nia ya kumchukua (Mirror)
Inter Milan itatoa muda wa wiki nyingine moja kujaribu kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta kabla ya kusonga mbele kwa malengo mengine. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Roma wamemtoa kiungo Manu Kone kwa Inter Milan, ambao wanatafuta makataba wa takriban euro milioni 30 (£26m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 24. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Uhamisho wa Liverpool kwa mlinzi wa Parma Giovanni Leoni unausisha pia timu hiyo ya Serie A kuwa na kipengele cha 10% cha mauzo katika mkataba wa Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 18. (Sky Sports Italia -in Italian)