BARCELONA: Mshambuliaji mpya wa Barcelona Marcus Rashford na kipa Joan Garcia wamefanikiwa kusajiliwa kwa wakati ili kuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa mabingwa hao wa LaLiga dhidi ya Mallorca baadae leo Jumamosi.
Barca ilitangaza kwamba Rashford na Garcia wote ni sehemu ya kikosi cha Hansi Flick kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea Mallorca. Rashford alisajiliwa mwezi uliopita kutoka Manchester United kwa mkopo akiwa na chaguo la kumnunua, huku Garcia akijiunga kutoka Espanyol mwezi Juni.
Kutokana na matatizo ya kifedha, Wakatalunya hao wamekuwa wakihangaika kusajili wachezaji, wakiwa wametumia pesa nyingi zaidi katika usajili na mishahara kuliko mapato waliyopata kwa misimu mingi iliyopita.
Wasifu wa Rashford na Garcia sasa zimeorodheshwa kwenye tovuti ya LaLiga, ingawa zile za Gerard Martin na kipa Wojciech Szczesny hazipo, ikidokeza kuwa Barcelona wanaweza kufanya usajili wa kuungaunga ikiwa hawawezi kukamilisha sajili zote kwa pamoja.
Barca walipata ahueni ya matatizo yao ya usajili baada ya mazungumzo ya ndani yaliyohusisha ushawishi kwa nahodha wao Marc-Andre ter Stegen.
Awali kipa huyo Mjerumani alikataa kusaini mkataba wa likizo ya muda mrefu ya matibabu ambao ungeondoa asilimia 80 ya mshahara wake na kusaidia klabu kufuata sheria za kifedha.
Akiwa nje kwa angalau miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji, Ter Stegen alipoteza unahodha kabla ya kuupata tena baada ya kukubaliana na mpango huo.
The post Barça yawawahi Rashford, Garcia first appeared on SpotiLEO.