MUNICH, WINGA wa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich Kingsley Coman yuko mbioni kujiunga na Klabu ya Al -Nassr Saudi Arabia klabu yake ikithibitisha mazungumzo ya usajili huo kuwa katika hatua za mwisho.
Coman mwenye umri wa miaka 29, Mwana-fainali wa Kombe la Dunia la 2022 na timu ya taifa ya Ufaransa amekuwepo Bayern kwa miaka 10, akishinda mataji ya ndani na ya kimataifa, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Dunia la Klabu.
Bayern hata hivyo walipata kigugumizi kuzungumzia kizungumkuti cha dili la kiungo mshambuliaji wa Stuttgart Nick Woltemade wakisema suala hilo linakuzwa na kuchochewa na Vyombo vya Habari nchini humo kufuatia kukataliwa mara kadhaa kwa ofa zao kwa mchezaji huyo.
Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern Christoph Freund amewaambia waandishi wa Habari kuwa bado kuna mazungumzo ya mwisho yanaendelea na dili hilo halijakamilika Lakini ni suala ambalo litatokea kwakuwa wapo katika hatua nzuri.
Kwa upande wa Kocha wa Bayern Vincent Kompany amesema kuondoka kwa Coman kunaweza kuwa kumetokana na hisia kukija muda mfupi baada ya klabu hiyo kumuaga mkongwe Thomas Mueller aliyehamia MLS kwenye klabu ya Vancouver Whitecaps baada ya miaka 25 klabuni hapo.
The post Coman njia nyeupe Saudi Arabia first appeared on SpotiLEO.