MANCHESTER: KIPA wa mabingwa wa Ulaya Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma, ameelekeza malengo yake ya kujiunga na klabu ya Manchester City katika dirisha hili la usajili. Hatua hii inakuja baada ya Manchester United kujitoa rasmi katika harakati za kumsajili kipa huyo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya England Manchester City kwa sasa inatafuta kuongeza nguvu katika safu yao ya ulinzi, hususan kutokana na uwezekano wa kufanya mabadiliko ya muda mrefu katika nafasi ya golikipa namba moja.
Donnarumma mwenye miaka 26 ambaye amekuwa PSG tangu mwaka 2021 baada ya kuondoka AC Milan, anatajwa kuvutiwa na ufundi wa Pep Guardiola na nafasi ya kucheza kwenye moja ya ligi ngumu zaidi duniani, Premier League.
Donnarumma amejizolea umaarufu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuokoa michomo, utulivu langoni, na uzoefu wa kucheza kwenye mashindano makubwa kama EURO 2020, ambapo aliiwezesha Italia kutwaa ubingwa na kutangazwa Mchezaji Bora wa Mashindano.
Iwapo dili hili litatimia, litakuwa moja ya usajili mkubwa wa kiangazi na linaweza kuathiri pakubwa mustakabali wa mlinda mlango wa sasa wa City, Ederson Moraes.
The post Donnarumma Kimeeleweka Man city first appeared on SpotiLEO.