MANCHESTER: Mabingwa wa zamani wa Ligi kuu ya England Manchester City wanaelekea katika msimu mpya huku wingu la kesi zao 115 likiwa bado linatanda juu yao na maswali kuhusu jinsi wachezaji wao wapya waliosajiliwa watakavyoingia haraka kwenye kikosi na kuisaidia timu hiyo kurejesha makali yake.
Wakiwa wametawala soka la England kwa misimu minne na kutwaa mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu, kikosi kilichoshinda kila kitu cha Pep Guardiola kilipitia tanuru la moto na msimu wa kukatisha tamaa wa 2024-25.
Katika msimu huo Man City walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakamaliza bila kombe lolote kubwa na kutolewa katika hatua ya 16 bora ya kwa Kombe la Dunia la Klabu kwa mshtuko na Al-Hilal ya Saudi Arabia.
City watakuwa kama mnyama aliyejeruhiwa, lakini bado kuna maswali mengi ya jinsi watakavyokabiliana na majereha ya msimu uliopita na kama Guardiola anaweza kutengeneza kikosi kingine tishio na kurejea kwenye mbio za ubingwa.
“Tuko tayari, tulikuwa na maandalizi mafupi ya ‘pre-season’ lakini yalikuwa mazuri sana na tuko tayari kufurahia wakati mzuri na kurejea kwenye ubora wetu haraka iwezekanavyo”
“Siwezi kukuhakikishia, lakini dalili ni kwamba tunaweza kuwa bora zaidi au labda wabovu zaidi. Huwezi kujua. Lakini nadhani itakuwa bora zaidi.” Pep Guardiola alisema
The post Maswali tele Man City ikianza msimu mpya leo first appeared on SpotiLEO.