Mratibu wa UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Via vya Uzazi na Homa ya Ini Mkoa wa Kigoma, Dkt. Hosea William akielezea namna Serikali na THPS wanavyoshirikiana kupambana na maambukizi ya VVU
Mratibu wa UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Via vya Uzazi na Homa ya Ini Mkoa wa Kigoma, Dkt. Hosea William akielezea namna Serikali na THPS wanavyoshirikiana kupambana na maambukizi ya VVU
Mratibu wa UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Via vya Uzazi na Homa ya Ini Mkoa wa Kigoma, Dkt. Hosea William akielezea namna Serikali na THPS wanavyoshirikiana kupambana na maambukizi ya VVU
Huduma za utoaji elimu na upimaji wa VVU zikiendelea kutolewa katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma
Huduma za utoaji elimu na upimaji wa VVU zikiendelea kutolewa katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma
Huduma za utoaji elimu na upimaji wa VVU zikiendelea kutolewa katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani KigomaMuelimishaji rika kutoka Kituo cha Afya Gungu, Abeda Ramadhani Ibrahim akielezea namna wanavyotoa huduma za Upimaji VVU katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma ili kuwafikia wavuvi na wananchi wanaofika katika Bandari hiyo yenye mwingiliano wa watu wengi.
Huduma za utoaji elimu na upimaji wa VVU zikiendelea kutolewa katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma
Mnufaika wa huduma za dawa kinga, Hadija Ramadhan akielezea faida za PrEP
Msimamizi wa Huduma za Jamii wa Mradi wa Afya Hatua mkoani Kigoma, Yethero Mgale akielezea kuhusu kampeni maalumu za huduma za afya katika Bandari ya Kibirizi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma
Na Kadama Malunde – Kigoma
Mradi wa Afya Hatua, unaotekelezwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (U.S. CDC), kwa kushirikiana na Timu za usimamizi wa afya za mkoa na halmashauri (RCHMT), umeendelea kufanikisha upatikanaji wa huduma za kinga, tiba na matunzo ya VVU kwa makundi yenye hatari kubwa ya maambukizi mkoani Kigoma.
Makundi hayo yanajumuisha wavuvi, wasichana rika balehe na wanawake vijana, watoto wa kina mama wanaoishi na VVU, madereva wa malori ya masafa marefu, pamoja na watu wanaojidunga dawa za kulevya na watu wanaoishi na VVU (WAVIU).
Mradi wa Afya Hatua unatekeleza shughuri zake katika ngazi za vituo vya afya na jamii. Kwa kushirikiana na Kituo cha Afya Gungu kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma-Ujiji, mradi unaendesha kampeni maalumu za huduma za afya katika Bandari ya Kibirizi zikilenga kufikia makundi yalio katika hatari ya kupata maambukizi.
Kuanzia Oktoba 2024 hadi Juni 2025, mradi umefanikiwa kuwapima VVU walengwa 224, ambapo 9 walibainika kuwa na maambukizi na wote kuunganishwa katika huduma ya tiba na matunzo, kusambaza vitepe 1,901 vya kujipima VVU (HIVST) na kuunganisha watu 44 katika huduma za dawa za kinga (PrEP).
Msimamizi wa Huduma za Jamii wa Mradi wa Afya Hatua mkoani Kigoma, Yethero Mgale, amesema kampeni hizi zinatoa huduma ya upimaji na ushauri nasaha wa VVU, usambazaji wa vifaa vya kujipima VVU (HIVST), huduma za PrEP, elimu na usambazaji wa kondomu.
“Hadi sasa, Kituo cha Afya Gungu kimewasajili mabinti 187 wanaojihusisha na biashara ya ngono na kuwaunganisha katika huduma ya dawa kinga (PrEP),” amesema Mgale.
“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni kuhamahama kwa walengwa wakifuatilia maeneo yenye shughuli za uvuvi”, ameeleza.
Ameongeza kuwa matumizi ya dawa kinga yamechangia kushuka kwa kiwango cha maambukizi ya VVU mkoani Kigoma hadi asilimia 1.7, lengo likiwa kufikia sifuri ifikapo mwaka 2030.
Muelimishaji rika kutoka Kituo cha Afya Gungu, Abeda Ramadhani Ibrahim, amesema ushiriki wa waelimishaji rika katika kusambaza vifaa vya kujipima VVU umeongeza idadi ya watu wanaotambua hali zao na kusaidia kugundua maambukizi mapya.
“Kila wiki tunawafikia zaidi ya watu 30 wanaofanya shughuli za uvuvi katika Bandari ya Kibirizi. Tunatumia mtandao wa marafiki ili kuwafikia wengi zaidi,” amesema.
Huduma hizo pia zinajumuisha elimu kuhusu kifua kikuu (TB), magonjwa ya ngono (STI), saratani ya mlango wa kizazi, matumizi ya PrEP na usambazaji wa kondomu.
Hadija Ramadhani, mmoja wa wanufaika wa dawa kinga (PrEP), amesema dawa hiyo imemlinda dhidi ya maambukizi ya VVU tangu aanze kuitumia na amewasihi mabinti wengine walio hatarini kuikubali na kuitumia.
Mratibu wa UKIMWI, Magonjwa ya Ngono, Via vya Uzazi na Homa ya Ini mkoa wa Kigoma, Dkt. Hosea William, amesema mchango wa THPS kupitia mradi wa Afya Hatua umeiwezesha serikali kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 3.4 mwaka 2012 hadi asilimia 1.7 mwaka 2024.