NIGERIA: MUIGIZAJI maarufu wa Nollywood Olusegun Akinremi, anayejulikana kitaalamu kama Chief Kanran, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.
Mtengenezaji wa filamu maarufu, Seun Oloketuyi, alitangaza kifo cha muigizaji huyo katika chapisho lake kwenye ukurasa wa Instagram.
“Muigizaji maarufu, Segun Remi amefariki …,” aliandika.
Wakati wa kuwasilisha ripoti hii, maelezo kuhusu kifo chake yalikuwa bado yana utata.
DAILY POST inaripoti kwamba Chief Kanran, ambaye alikuwa maarufu katika tasnia ya filamu ya Kiyoruba, alijulikana kama Jenerali Philips katika sehemu ya 13 ya tamthilia iliyokuwa ikioneshwa kwenye TV ya Megafortune.
The post Muigizaji Nigeria Chief Kanran afariki dunia first appeared on SpotiLEO.