DARES SALAAM: RAPA kutoka Tanzania Frida Amani ni miongoni mwa wanamuziki walioharikwa kutumbuiza katika Tamasha la siku mbili la muziki litakalofanyika katika Jiji la Tshwane, nchini Afrika Kusini kuanza Oktoba 30 hadi Novemba 1,2025.
Wasanii wengine wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni wasanii kutoka Afrika ya Kusini Focalistic, Thakzin, Naledi Aphiwe, Shandesh, The Charles Géne, Njoki Filingo, Bokani Dyer na Jabulile Majola.
Wengine ni Boukuru kutoka Rwanda, Mwendamberi kutoka Zimbabwe, Tobi Peter kutoka Nigeria, Claudio & Rabe kutoka Madagascar, Karu Sebina kutoka Botswana na Oumy kutoka Senegal.
Tamasha hilo toleo la 8 la Muziki Barani Afrika linaloleta Ushirikiano, Mabadilishano na Maonesho mbalimbali, kupitia kongamano lake kubwa linatarajiwa kuleta fursa za mitandao kuendesha warsa na utoaji wa tuzo kwa washiriki mbalimbali.
Kongamano hilo linatarajiwa kuwa na zaidi ya wajumbe 1,000 waliohamasishwa kutoka zaidi ya nchi 45.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa Kongamano hilo, shughuli za mkutano zitaendeshwa katika Ukumbi wa Michezo wa Aula, Chuo Kikuu cha Pretoria, Agosti 30 na 31 Oktoba ikishirikisha zaidi ya wazungumzaji 60 kutoka katika tasnia ya muziki duniani kote.
“Taarifa hiyo ilitangaza kundi la kwanza la wazungumzaji katika Kongamano hilo kuwa ni: Meneja wa Kimataifa wa Mradi kutoka CNM nchini Ufaransa Benjamin Demelemester, Meneja Uhusiano, Sanaa katika British Council kutoka Uingereza Kwame Safo na Mkurugenzi Mtendaji wa SAMPRA kutoka Afrika Kusini Pfanani Lishivha.
Wengine ni Shiba Melissa Makeda kutoka Afrika Kusini, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Grown Kid kutoka Ufaransa Cécilia Pietrzko na Mkurugenzi wa Tamasha kutoka MTN Bushfire Eswatini Mount Maza.
The post Rapa Frida Amani kutumbuiza Afrika Kusini first appeared on SpotiLEO.