MADRID: Meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu pendekezo la kucheza mechi ya LaLiga nchini Marekani dhidi ya Barcelona, akisema ni mapema mno kuwa na wasiwasi kuhusu ubaya wa matokeo ya pendekezo hilo.
Jirani zao Real Madrid wamepinga vikali pendekezo la kuhamishia mechi zao za mwezi Disemba dhidi ya Villarreal na Barcelona jijini Miami, pendekezo ambalo liliidhinishwa na shirikisho la soka la Hispania Jumatatu, ingawa bado halijaidhinidhwa na UEFA, mamlaka za Soka la Marekani, CONCACAF na FIFA.
“Nado ni mapema mno. Tunakuwa na wasiwasi kila wakati kuhusu mambo ambayo mara nyingi hayatokei. Tunajichosha kwa mambo ambayo tunajua wazi hayafanikiwi,” Simeone aliwaambia waandishi wa habari leo Jumamosi kuelekea mchezo dhidi ya Espanyol mchezo wao wa ufunguzi wa LaLiga msimu huu.
Atletico, ambao walishinda taji la Laliga mara ya mwisho mwaka 2021, wanapigania upya taji hilo baada ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita, wakitumia zaidi ya euro milioni 150 ($175.46 msimu huu kuboresha kikosi chao.
The post Simeone akingia kifua mechi nje ya nchi first appeared on SpotiLEO.