Kiungo mkongwe, Haruna Niyonzima, amefunguka mazito juu ya mastaa wa Simba SC na dira ya klabu hiyo, akisisitiza kuwa chini ya uongozi wa bilionea Mohammed Dewji (Mo), Wekundu wa Msimbazi wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Afrika.
Niyonzima, ambaye amewahi kuchezea klabu kubwa nchini, amesema Simba imebadilika na ina mipango mikubwa inayofanywa kwa vitendo na sio maneno matupu.
“Mo Dewji ni kiongozi tofauti, ni mtu anayeipenda Simba kwa dhati. Namjua, anataka kuona timu hii ikifikia kilele cha mafanikio barani Afrika. Ukiangalia uwekezaji anaoufanya ni wazi kabisa malengo yake ni kombe la Afrika,” alisema Niyonzima.
Mkongwe huyo ameongeza kuwa uwezo wa kifedha, maandalizi ya kisasa, pamoja na wachezaji wanaosajiliwa kila msimu vinaonyesha wazi Simba ipo kwenye njia sahihi ya kuandika historia kubwa barani.