#TETESI: Aliyekuwa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ amejiunga na klabu ya Simba Sc kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Wydad Casablaca inayoshiriki ligi kuu Nchini Morocco.
Gomez ambaye alijiunga na Wydad mwishoni mwa msimu uliopita anarejea Tanzania kwa mkopo huku akitarajiwa kuungana na mshambuliaji mwenzake Jonathan Sowah ambaye naye alikuwa Singida Black Stars.
Mwalimu alikuwa sehemu ya kikosi cha Wydad Casablanca kilichoshiriki michuano ya kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu huko Marekani ambapo alicheza mechi mbili kati ya tatu za hatua ya makundi.