DAR ES SALAAM: KLABU ya Tanzania Prisons imemtambulisha rasmi mlinzi mpya Heritier Lulihoshi, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Lulihosho amekuwa akicheza soka la ushindani katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kabla ya kujiunga na Prisons, alikipiga Dodoma Jiji FC, na pia aliwahi kuchezea Tabora United na Musanze ya Rwanda, ambako aliweka msingi wa kipaji chake.
Ujio wake katika kikosi cha “Wajelajela” unalenga kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo, huku akitarajiwa kuongeza kasi, ukakamavu na uzoefu wa kimataifa ndani ya kikosi.
Wakati ikiongeza nguvu, Prisons pia imewapa mkono wa kwa heri nyota wake wawili waliokuwa sehemu ya kikosi kwa misimu kadhaa, Beno Ngasa na Vedastusi Mwihambi, ambao wamemaliza rasmi muda wao ndani ya klabu hiyo ya Jeshi la Magereza.
Uongozi wa klabu hiyo umewashukuru wachezaji hao kwa mchango wao mkubwa na kuwatakia kila la heri katika safari zao mpya za kisoka.
The post Prisons yatambulisha mashine mpya first appeared on SpotiLEO.