“Hii ndiyo sababu hasa hatukutaka Bafana Bafana washiriki CHAN tangu mwanzo.
Tulitaka kushiriki AFCON tu. CAF walituambia hatuwezi kuchagua mashindano tunayoshiriki, tukawaheshimu.”
Tulichukua hatua ya haki… lakini bado wametutendea vibaya. Sasa wanakuja kutuambia kwamba wamesimamisha marefa… Hapana! Hatutashiriki CHAN tena, ni AFCON tu!”
Rais wa SAFA, Dkt. Danny Jordaan, baada ya kutolewa kwa Afrika Kusini kwenye mashindano ya CHAN kufuatia sare ya 3-3 dhidi ya Uganda.