“Tunashukuru wadhamini ambao wanawekeza kwenye maendeleo halali ya Mpira, hatuwezi tukatumia pesa zinazotolewa na wadhamini kwenye maendeleo yasiyo halali Kwenye Mpira ,kwahiyo Mpira una njia zake “
“Rais wa Yanga, ni Ndugu yangu,rafiki yangu,kila tukikaa ananieleza haja ya Yanga kuwa na uwanja wake mkubwa,na mimi napata bahati kidogo pengine kuliko mtu mwingine ananionesha viwanja vingi sana kwenye laptop yake, kwahiyo kila akinifungulia namwambia Rais usitujengee kwenye laptop Yanga inahitaji miundombinu ya kweli “
“Kwahyo wakati tunazungumzia maendeleo ya Mpira, lazima tuzungumzie maendeleo ya miundombinu ya Mpira, wakati tunazungumzia mafanikio ya kuuza wachezaji wetu, hatuwezi kutengeneza wachezaji bila kuwa na hiyo miundombinu ya Mpira “
“Kwahiyo Rai yetu sisi kwa Viongozi wa vilabu nyetu vyote nikwamba, tutumie hizi fursa za wadhamini katika kujenga, miundombinu ya Maendeleo ya mchezo wenyewe “
“Haiwezi kuwa fahari yetu, tukatumia pesa nyingi tunazopata kwenye udhamini,pesa ambazo hazitoshi tukawa tunazitumia kuingia gharama kubwa ya kununua wachezaji, wakati sisi tunaamini kwamba ,nchi yetu ina vipaji vya kutosha inao wachezaji wakutosha”
“Tunaweza tukatengeneza wakina Clement Mzize wengi sana, msimu kama huu tukapata habari hapa kwamba, Yanga SC imeuza wachezaji 20 au 30, kwasababu ina benki kule ya Vijana wenye vipaji ” amesema makamu wa Rais wa TFF Athuman Nyamlani.