Na Vero Ignatus Arusha.
Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuanzisha na kuendeleza madawati ya sheria,yatakayo wasaidia kuwaondoa waandishi wa habari kuingia katika makosa ya kisheria kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Rai hiyo imetolewa leo Agosti 20,2025 Kijijini Arusha na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ernest Sungura,katika mafunzo na msaada wa kisheria kwa waandishi wa habari mkoa wa Arusha,na kusisitiza kuwa madawati ya kisheria yatasaidia kuwa na habari zisizo vunja sheria.
Sungura amesema wakati mwingine kunamahojiano yanafanyika kwa ushauri wa mawakili ili kumuondoa mwandishi kuingia kwenye udhalilishaji au uchochezi utakaomuingiza matatani.
“Maisha yako yanathamani kubwa kuliko kazi yako hiyo, kwa kuwepo na dawati la ushauri wa kisheria kunasaidia sana kwa chombo au mwandishi kutokuingia matatani”alisema Sungura.
Sambamba na hayo Uongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha APC,kwa kupitia mwenyekiti wao Cloud Gwandu umesema kuwa mafunzo hayo yatasaidi wanachama wake kuwa salama wanapokuwa wakitekeleA majukumu yao ,hasa kwa kuzingatia uwepo wa sheria mbalimbali za uchaguzi kabla na baada ya zoezi la kupiga kura.
Aidha Gwandu amewataka waandishi wote waliopata mafunzo hayo kuhakikisha wana kuwa mfano Bora wa kuigwa katika utendaji wait.
Julius Msagati ni mmoja wa washiriki katika mafumzo hayo ya siku moja amesema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia kufahamu haki yake na wajibu wake Kikatiba na kujua sheria sambamba na kuitekeleza.
“Mimi kama muandishi wa habari mafunzo haya ni muhimu kwangu kwani yameniwezesha kupata Elimu pana juu ya kuijua sheria na kuitekeleza,kutoka na ukweli kwamba yapo makosa ambayo tumekuw tukiyafanya na kupelekea habari zetu kuathiri upande wa jamii na kuacha taharuki ama kwa upande mwengine kutuingiza hatiani. Hivyo Elimu hii imekuja mahala sahihi, kwa wakati sahihi na kwa kundi sahihi”
Kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa madhila kwa waandishi na vyombo vya habari iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ya mwaka 2020,waandishi wa habari na vyombo vya habari 40 walikumbwa na madhila mbalimbali, Jiji la Dar es salaam ikiongoza na Jiji la Arusha ikiwa nafasi ya pili.