Simba kupoteza mchezo wa kirafiki ni faida kubwa sana kwao kwa sababu itamsaidia kocha Fadlu Davids kujua changamoto zilizosalia kwenye timu yake na kuzifanyia kazi.
Pia itamsaidia kujua ni eneo gani uwanjani halijakamilika kwa maana ya wachezaji na kumpa room ya yeye kwenda kusajili wachezaji wengine kabla dirisha la usajili halijafungwa.
Inamsaidia pia kwenye maswala ya fitness kama wachezaji wake hawajafikia level anayoitaka basi aongeze dozi kwa wachezaji wafikie level anayoitaka.
Pia kocha anaepuka kutumia nguvu kubwa ambazo zitawasababishia wachezaji wake uchovu kabla ya msimu husika kuanza hivyo hawawezi kutumia nguvu kubwa kwenye mchezo wa pre season.
Hivyo kwa kocha Fadlu inamsaidia sana Simba wakipoteza mchezo wa Pre season kwa sababu inamsaidia kuiandaa timu yake vizuri kuelekea msimu ujao.